1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwendesha Mashitaka wa Afrika Kusini Mkwebane yuko matatani

Amina Mjahid Mohammed Khelef
22 Julai 2019

Mahakama ya katiba nchini Afrika Kusini imetoa uamuzi wake kwamba mwendesha mashitaka aliyemtuhumu Rais Cyril Ramaphosa kwa kuwa na uongozi mbaya, alichukua hatua hiyo akiwa na nia mbaya dhidi ya rais huyo

https://p.dw.com/p/3MYOS
Adv Busisiwe Mkhwebane
Picha: Getty Images/AFP/P. Magakoe

Uamuzi huo unaweza kutilia mashaka uaminifu wa mwendesha mashitaka Busisiwe Mkhwebane, aliyekuwa akichunguza kisa cha kuchochea uchumi kilichofanyika wakati wa enzi za ubaguzi wa rangi.

Kwa sasa Mkwebane anajitayarisha kwenda mahakamani dhidi ya Rais Ramaphosa na Waziri wa Biashara Pravin Gordhan, ambaye ni mshirika muhimu wa rais.

Südafrika Präsident Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: Reuters/R. Bosch

Mahakama ya katiba imesema Busisiwe Mkhwebane hakuwa muwazi kuhusu shughuli zake wakati wa uchunguzi.

Mahakama hiyo sasa imethibitisha adhabu dhidi ya Mkhwebane iliyotolewa na mahakama ya juu mwaka uliopita kwa kutumia njia zisizo sawa katika uchunguzi aliyoufanya mwaka 2017.

Benki ya Akiba ya Afrika Kusini ilipinga mapendekezo aliyoyatoa Mkhwebane katika kesi hiyo, na kutaka  madaraka yake yabadilishwe kama hatua za mara moja zinazopaswa kuchukuliwa dhidi yake na pia alitakiwa kulipia gharama za kisheria.

Hata hivyo, mwendesha mashitaka huyo amesema ni lazima auangalie uamuzi kwa makini kabla ya kuzungumza chochote.

Mkhwebane ashutumiwa kuungana na wale wanaomuunga mkono rais  Zuma

Kabla ya uamuzi wa leo, jana Jumapili RaisRamaphosaalisema atamfikisha mahakamani Bi Mkwebane kupinga matokeo ya uchunguzi wake dhidi yake, kwamba alilipotosha bunge kuhusu mchango wake katika kampeni za urais za mwaka 2017 alipokuwa anawania uongozi wa chama tawala Afrika Kusini, ANC.

Joyce Busisiwe Mkhwebane Public Protector Official Photo
Mwendesha mashitaka wa Afrika Kusini Busisiwe MkhwebanePicha: GCIS

Wakati huo huo wafuasi wa Rais Ramaphosa wanamshutumu Mkhwebane  kwa kujiunga na vita vya chini kwa chini vya wale wanaomuunga mkono rais wa zamani, Jacob Zuma, madai ambayo anayakanusha vikali.

Uchunguzi mwengine wa hivi karibuni uliofanywa na Mkhwebane uligundua kuwa Waziri wa Biashara Pravin Gordhan alikiuka katiba kwa kuongeza madaraka yake wakati alipokuwa kamishna wa ushuru.

Gordhan, aliyewahi pia kuwa waziri wa fedha, anayakana matokeo ya uchunguzi huo. Kwa sasa anasimamia juhudi za kufufua kampuni kadhaa za serikali kama shirika kubwa la umeme nchini Afrika Kusini, Eskom, na kampuni ya kutengeneza silaha ya Denel.

Vyanzo: Amina Abubakar/Reuters/afp/dpa