1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwisho wa madeni ya Ujerumani unakaribia

Charo, Josephat1 Julai 2008

Baada ya miongo minne ya sera za kujilimbikizia madeni, bajeti ya Ujerumani inaelekea kuchukua mkondo mpya wa kutokuwa na madeni yoyote.

https://p.dw.com/p/EUOr
Ujerumani inakabiliwa na deni la euro bilioni 900Picha: AP

Kulingana na pendekezo la bajeti ya serikali ya mwaka ujao 2009 na mpango wa matumizi ya fedha hadi mwaka 2012 inawezekana kufikia lengo la kutokuwepo madeni mapya kiurahisi kuliko vile ilivyokuwa ikihofiwa hapo awali.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Peer Steinbrück amefaulu baada ya mzozo wa miezi kadhaa kupitisha mpango wake wa kubana matumizi ya fedha na kuzuia mipango ya matumizi ya mawaziri wenzake. Wazo la waziri wa fedha Peer Steinbrück linatarajiwa kujadiliwa leo na baraza la mawaziri mjini Berlin.

Lengo kubwa linaonekana kukaribia kufikiwa. Mwisho wa miongo kadhaa ya kujilimbikizia madeni katika serikali unakaribia kufikiwa ifikapo mwaka wa 2011.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka 40, bajeti ya Ujerumani haitaweza tu kugharamiwa kutoka kwa kodi inayokusanywa pekee, bali pia kuanza kulipa madeni ya kiasi ya euro bilioni 900. Hilo ni muhimu sana kwa kuwa kwa kipindi kirefu serikali imekuwa na mzigo mkubwa kuvigharamia vizazi vya kesho vya Wajerumani.

Gharama ya kushughulikia malipo ya madeni imefikia euro bilioni 42 hivyo kuwa deni la pili kwa ukubwa katika bajeti na kutishia kupunguza uwezo wa kisiasa wa serikali kuendesha shughuli zake.

Katika miaka yote miwili ijayo waziri wa fedha wa Ujeumani anataka kukopa madeni kwa kuwa anataka kusawazisha bajeti. Na katika miaka mingine itakayofuata hataki tu kuanza kulipa madeni, bali pia raia wanatakiwa wanufaike kutokana na kupunguzwa kwa kodi kutokana na bajeti iliyoimarika.

Bajeti inatarajiwa kusawazika ifikapo mwaka wa 2011 kutokana na mapato ya mauzo ya mali ya serikali ya thamani ya euro bilioni tano na katika mwaka huo takriban euro bilioni mbili.

Hali ya bajeti ya serikali ni ya wasiwasi na itaendelea kubakia hivyo kwa muda. Hayo pia yanahusiana na kwamba serikali ya muungano imelipa kipaumbele swala la kurejea kwa haliy a kawaida ya bajeti yake kiasi kwamba haiwezi kuwekea mipaka sera zake peke yake.

Serikali inalazimika kuwekeza katika kuijenga upya miundombinu hasa ya barabara. Matumizi katika utafiti na uvumbuzi yanatakiwa yaongezeke ili Ujerumani iweze kukabiliana na mashindano makali na kuilinda nafasi yake katika ngazi ya kimatiafa au iiboreshe.

Serikali inatakiwa iongeze matumizi kwa ajili ya familia na watoto ili kuhakikisha usalama wa siku za usoni wa taifa hili na inatakiwa igharamie majukumu yake ya kimataifa. Kwa hilo sio tu wanajeshi wa Ujerumani walio nchini Afghanistan na mataifa ya Balkan bali pia ushirikiano wa kimaendeleo.

Na hatimaye ni vita dhidi ya baa la njaa. Vifo vya watoto na ukosefuw a elimu kwa watoto, sio tu kwa sababu za kibinadamu bali kwa maslahi ya kibinafsi ikiwa mabadiliko ya haliy a hewa yatapigwa vita au kupitia kuimarisha uchumi wa nchi maskini kuweza kupunguza tatizo la uhamiaji.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ndio maana ameahidi kuongeza fedha kwa ajili ya maendeleo. Katika bajeti ya serikali matumizi yataongezeka kwa asilimia 1.8 mwaka ujao,lakini katika wizara ya maendeleo kumepangwa kuwa na nyongeza ya asilimia 12,4 ambayo ni kiasi cha euro bilioni 5,8.

Hizo ni fedha nyingi lakini hazitoshi kufikia kiwango cha asilimia 0.51 mwaka wa 2010 kilichoahidiwa na kansela Merkel kwa ajili ya ushirikiano wa kimaendeleo. Katika miaka ijayo kiwango hiki kitapanda kwa asilimia0.38. Hilo pia litategemea kukua kwa uchumi na pia masilahi muhimu ya kisiasa.

Tayari kuna uwezekano wa raia kupunguziwa kodi katika mwaka ujao wa uchaguzi na wanatarajiwa kuahidiwa kupunguziwa kodi kwa kiwango kikubwa. Hilo ni muhimu zaidi kwa vyama katika serikali, kansela na waziri wa fedha kuliko kuweka tayari fedha kwa ajili ya ushirikiano katika shughuli za kimaendeleo.