1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwisho wa Marekani kuikalia Iraq kwa idhini ya UN mwakani

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTi2

BAGHDAD.Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki amesema kuwa mwaka ujayo utakuwa ni mwisho kwa majeshi ya Marekani kuendelea kuwepo nchini humo chini ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa.

Baada ya hapo Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa majeshi hayo yatakaa huko kutokana na mkataba mpya utakaofikiwa kati ya Marekani na Iraq.

Nuri al-Maliki na Rais George Bush walikubaliana azimio litakalowaelekeza katika mazungumzo ya kuanzishwa kwa uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Marekani imesema kuwa mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza mapema mwakani na kumalizika mwezi Julai.