1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

201210 Elfenbeinküste Wahlen

21 Desemba 2010

Vizuizi, kuchomwa moto matairi ya magari na mapigano makali mitaani, ni picha iiliyojitokeza mjini Abidjan na katika majimbo mengine, ikikumbusha mapigano ya silaha yaliporipuka kuanzia mwaka 2000 nchini Ivory Coast

https://p.dw.com/p/QhB0
Mapigano katika mitaa ya jiji la AbidjanPicha: AP

Hali zote hizo mbili za mapigano ya wakati huo na sasa hivi kimsingi zinafanana.Nani ananyemuunga mkono Ouattar?Katika uchaguzi wa urais wa tarehe 28 mwezi uliyopita, tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza Alassane Ouattar kuwa mshindi.Lakini tangazo hilo ambalo kikatiba ni halali, lilipingwa na Gbagbo na wafuasi wake wakajitangazia ushindi kinyume na sheria

Elfenbeinküste Wahl Alassane Ouattara
Kiongozi wa upinzani Alassane OuattaraPicha: AP

Alassane Ouattara anafaidi uungwaji mkono kwa kiwango kikubwa na jumuiya ya kimataifa.Alijipatia Sifa na heshima nzuri wakati alipokuwa Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF pamoja na Waziri Mkuu wa Ivory Coast katika miaka 90.Ouattara ni mwanadiplomasia na mwanasiasa mwenye uzoefu.Familia yake inatoka katika eneo la kaskazini:

Ndiyo maana Ouattara au ADO kama anavyojulikana na wafuasi wake, anaungwa mkono na watu kutoka eneo hilo la kaskazini pamoja na maeneo ya katikati mwa Ivory Coast.

Katika uchaguzi wa mwaka 2000 Ouattara hakuruhusiwa kushiriki kugombea.Alizuiliwa kwa hoja kuwa hakuwa raia wa Ivory Coast.Kigezo cha uzawa kilitumika mwishoni mwa miaka ya 90 katika kuwazuia watu ambao hawakutakiwa kuingia katika siasa kuwania uongozi, halikadhalika jeshini.

Hali hiyo imewafanya wananchi wa Ivory Coast kwa mara ya nne kukosa haki yao.Ndiyo maana Ouattara aliungwa mkono na kizazi cha pili cha wananchi wa Ivory Coast ambao ni wa kutoka nje, kupata haki yake ya uraia.Mzozo huu ulikuwa chanzo kikuu cha mgogoro, na kuanza kwa uasi mpya jeshini.

Mwaka 2002 waasi walianzisha mapambano dhidi ya utawala wa Gbagbo kutokea kaskazini kuelekea Abidjan.Kwa Gilles Yapi ambaye ni mtaalam wa masuala ya siasa ni muhimu kuelewa hali iliyopo hivi sasa.

´´Dai kuu kisiasa la wanajeshi waliyoanzisha uasi lilikuwa ni swala la kuhusiana na uraia.Kuna swali ni mgombea yupi kwa hakika anaruhusiwa na iwapo Alassane Ouattara anahusika.Hii ni kusema kikawa kigezo cha kuunganisha mapambano ya silaha ya waasi hao na yale ya kisiasa ya Ouattara katika kuwania haki yake ya uraia..“

Präsidentschaftswahlen Elfenbeinküste Laurent Gbagbo
Kiongozi wa Ivory Coast Laurent GbagboPicha: picture alliance/PANAPRESS/MAXPPP

Ngome ya Gbagbo iko kusini mwa nchi hiyo, ambako alijiimarisha tokea mwaka 2000, alipompindua aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Jenerali Robert Guei.Laurent Gbagbo alichukua uongozi na kuonekana kama tumaini jipya la upinzani dhidi ya mfumo wa chama kimoja.Jeremy Soukrou ni mmoja wa wafuasi wake ambaye aliandaa mdahalo wa kampeni za Gbagbo.

"Sote tunaunga mkono mpango wa Rais Gbagbo,ambao tuliuona unafaa.Na tuko tayari das wir richtig finden. Na tuko tayari kumuunga mkono, kuzilinda taasisi za nchi yetu na kutetea maisha yake kwa maana ya kwamba raia wa nchi yetu´´


Gbagbo amekuwa akiwapa zawadi za fedha pamoja na kuwapandisha vyeo jeshini, watu wanaomtii.Aidha kikosi maalum cha jeshi la nchi hiyo kinamuunga mkono.Kikosi hicho cha jeshi pia kinatumika kulinda taasisi za nchi hiyo.Kwa ujumla Gbagbo ameshika hatamu katika sehemu zote nyeti na muhimu .Lakini ili kuivuja nguvu hiyo ya Gbagbo ni kwa jumuiya ya kimataifa kuzidisha mbinyo na kumtenga.Tayari vikwazo kadhaa vimekwishatangazwa, ambapo Umoja wa Ulaya kwa mfano unatarajia kutangaza vikwazo vya kusafiri dhidi yake na mamafisa wake.

Mwandishi:Schaeffer, Ute/Blanchard, Sandrine/Aboubakary Liongo

Mhariri:Josephat Charo



Audio-Link:


ENDE