1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo katika chama cha NPD

Oumilkher Hamidou14 Aprili 2009

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia NPD chakabwa na mizozo

https://p.dw.com/p/HWZW
Mwenyekiti wa NPD Udo VoigtPicha: AP

Tetesi zimezagaa kuhusiana na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani-NPD.Chama hicho chenye wafuasi 7200 (kwa mujibu wa hesabu za mwaka 2007),kinaangaliwa kua chama kikubwa kabisa miongoni mwa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia humu nchini.Hata hivyo katika mkutano wake mkuu uliopita mjini Berlin,mvutano umezuka;Hali hiyo si nzuri kwa chama hicho hasa kwa mwaka huu wa 2009 uliogubikwa na chaguzi tofauti.

Kashfa za fedha,matokeo mabaya ya uchaguzi na lawama za ndani chamani ndio mitihani inayomzungusha kichwa mwenyekiti wa chama hicho cha siasa kali za mrengo wa kulia-NPD,Udo Voigt.Lakini anaendelea kushikilia wadhifa huo..Anajinata na kuzungumzia jinsi alivyofanikiwa kuchochea mjadala mkali uliodumu saa kadhaa wakati wa mkutano huo mkuu wa chama chake kwa kusema:

"Ni ishara kwamba chama kimepania kufanya kampeni kupigania viti katika chaguzi kadhaa za mwaka huu na hata katika kampeni za uchaguzi mkuu na nnamini,tuna nafasi nzuri ya kuingia katika mabunge ya majimbo matatu."


Hadi wakati huu NPD kimekua kikiwakilishwa katika mabunge ya majimbo mawili tuu;yaani katika jimbo la Sachsen kwa viti vinane na katika jimbo la Mecklenburg-Vorpommern kwa viti sita.


Kuchaguliwa tena mwenyekiti wa chama hicho Udo Voigt kwa asili mia 62 ya kura kunadhihirisha hata hivyo imani ya wafuasi wa NPD kwa mtaalam huyo wa masuala ya kisiasa mwenye umri wa miaka 56,,anaekiongoza chama cha NPD tangu mwaka 1996 imepungua.


Mtafiti wa masuala yanyohusu vyama vya kisiasa, Richard Stöss wa kutoka Chuo kikuu cha Freien Universität Berlin anatoa mfano wa malumbano yaliyozuka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha NPD na kusema:

"Tunajua kwamba mwenyekiti wa chama Udo Voigt amelaumiwa vikali lakini lawama hizo hazikua kali hivyo,na wafuasi hawakua wakamavu vya kutosha kuweza kumng'owa madarakani mwenyekiti wao na kumteuwa mtu mwengine."

Ingawa mpinzani wa Voigt chamani alikua Udo Pastör,mkuu wa NPD katika jimbo la Meclenburg-Vorpommern,alimpongeza mwenyekiti huyo aliyechaguliwa upya,hata hivyo lawama dhidi yake hazijesha.Sababu ya hayo ni kashfa ya fedha inayokidhoofisha chama chao.Mshika hazina anasemekana kutumia vibaya malaki ya yuro na kusababisaha vurugu katika hesabu za chama jambo lililopelekea chama cha NPD kutozwa faini ya yuro milioni mbili na nusu.

Muandishi Kiesel / Hamidou Oummilkheir

Mhariri Ramadhani Saumu