1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa gesi kumalizika ?

Abdu Said Mtullya8 Januari 2009

Urusi imesema ipo tayari kuanza tena kupeleka gesi barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/GUds
Mawaziri wakuu wa Urusi,Putin na wa Ukraine Tymoshenko.Picha: picture-alliance/ dpa

Kampuni ya gesi ya Urusi Gazprom imesema ipo tayari kuanza tena kupeleka gesi katika nchi za Ulaya haraka iwezekanayvo kwa sharti kwamba Umoja wa Ulaya unasimamia usafirishaji wa gesi hiyo kupitia Ukraine.Mkuruzgenzi wa kampuni hiyo Alexei Miller amesema hayo baada ya mazungumzo yake mjini Brussels.

Hapo awali hakuna kilichofikiwa kwenye mkutano wa dharura uliofanyika mjini humo mapema leo, badala yake mazungumzo mengine ya ana kwa ana yalifuatia baina ya wakuu wa kampuni za gesi ya Urusi,Gazprom na ya Ukraine Naftogaz. Mkuu wa kamati ya masuala ya nchi za nje kwenye bunge la Umoja wa Ulaya amesema kuwa wakurugenzi wa kampuni hizo walifanya mazungumo hayo ya ana kwa ana.

Hapo awali kikao cha dharura cha mjini Brussels kilichoitishwa kutokana na juhudi za Umoja wa Ulaya kilijadilli pendekezo la Umoja huo juu ya kupeleka wajumbe nchini Urusi na Ukraine kusimamia shughuli za usafirishaji wa gesi kwa ajili ya nchi za Ulaya.Mkuregenzi wa kampuni ya gesi ya Urusi Gazprom Miller alisema muda mfupi uliopita kuwa kampuni ya nchi yake Gazprom ipo tayari kuanza tena ugavi wa gesi kwa nchi za Ulaya chini ya sharti kwamba Umoja wa Ulaya unasimamia ugavi huo.

Mkutano wa ana kwa ana wa wakuu wa kampuni za gesi za Urusi na Ukraine umefanyika siku mbili baada ya Urusi kusimamisha ugavi wote wa gesi inayopitia katika mabomba ya Ukraine na hivyo kusabisha upungufu mkubwa wa gesi katika nchi kadhaa za Ulaya.Urusi ilisimamisha ugavi wa gesi kwa Ukraine kutokana na mgogoro wa kibiashara baina ya nchi mbili hizo. Urusi imesema kuwa Ukraine haijalipa malimbikizo ya deni lake.Urusi iliifungia bomba Ukraine.Urusi pia inadai kuwa Ukraine ilikuwa inaiba gesi . Kwa upande wake Ukraine imesema kuwa Urusi imeikatia gesi ili kusababisha mgogoro.

Katika juhudi za kuutatua mgogro huo Mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya Manuel Barroso pia amekutana na mkurugenzi wa kampuni ya gesi ya Urusi-Gazprom Alexei Miller na mkurugenzi wa kampuni ya Ukraine, Naftogaz Oleg Dubyna.

Wakati huo huo nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zimethibitisha kuwa hazipati gesi hata kidogo.Kamishana wa masuala ya viwanda wa Umoja wa Ulaya Günter Verheugen ameitaka Urusi itimize wajibu wake katika kupeleka gesi kwa wateja wake barani Ulaya.Amesema njia mojawapo ya kutatua mzozo huo wa gesi ni kupeleka wasimamizi watakaofuatilia shughuli za usafirishaji wa gesi kutoka Urusi na kupitia Ukraine.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia ametoa mwito wa kufikiwa suluhisho la haraka.