1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa gesi washika kasi Tanzania

Admin.WagnerD3 Januari 2013

Mzozo wa gesi ya Mtwara kusafirishwa jijini Dar es Salaam unazidi kufukuta, ambapo sasa madai hayo yanapata uungwaji mkono kutoka katika makundi mbalimbali ya watu wakiwemo viongozi wa dini na wasomi.

https://p.dw.com/p/17Cyk
Tanzania's President Jakaya Kikwete speaks during a press availability with Secretary of State Hillary Rodham Clinton at the State House in Dar es Salaam, Tanzania, Monday, June 13, 2011. (Foto:Susan Walsh, POOL/AP/dapd)
Rais wa Tanzania Jakaya KikwetePicha: dapd

Huku mzozo wa gesi ya mkoa wa Mtwara kusafirishwa jijini Dar es Salaam Tanzania ukizidi kufukuta, sasa baadhi ya wachambuzi nchini humo wanaungana na wakaazi hao wakisema kuwa wana madai ya msingi ya kutaka mkoa wa Mtwara moja kati ya mikoa maskini nchini humo kufaidika na mapato ya gesi hiyo kabla ya taifa zima kunufaika na rasilimali hiyo.

Awali waziri wa nishati na madini nchini Tanzania, Profesa Sospeter Muhungo, alisema haoni wakaazi hao wakiwa na madai ya uhakika. Muhongo alisema kulingana na katiba ya Tanzania rasilimali zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila ubaguzi kauli inayofanana ile iliyotolewa na rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya hivi karibuni.

Kwa kufahamu zaidi mzozo huo Amina Abubakar amezungumza na Gwandumi Mwakatobe ambaye ni Muandishi wa Habari na pia mchambuzi wa sisa za Tanzania. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini

Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Josephat Charo