1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa kisiasa Kenya

Ramadhani Yusuf, Saumu16 Februari 2008

Hakuna mwafaka wa kugawana madaraka uliofikiwa Kenya

https://p.dw.com/p/D8Nx

NAIROBI




Serikali ya Kenya na chama kikuu cha upinzani wamekubaliana  kuunda tume huru ya kuchunguza mgogoro wa matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka jana yaliyomrudisha madarakani rais Mwai Kibaki.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alitoa tangazo hilo baada ya kuongoza mazungumzo ya siku mbili juu ya suala hilo kati ya serikali na chama cha bwana Raila Odinga cha ODM.Aidha Kofi Annan  alikiri kwamba masuala yanayozungumziwa ni mengi na magumu lakini ana matuamini kwamba pande hizo mbili zinazozozana kuhusu madaraka zitaafikiana kuunda serikali ya mseto.Mazungumzo hayo ya suluhu yataanza tena jumanne ijayo.Matokeo ya uchaguzi wa rais hapo mwezi Desemba ambayo upinzani unasema yalikuwa ya uongo   yalizusha mapigano makali ya kikabila na kusababisha kuuwawa kwa watu zaidi ya 1000 nchini Kenya na kuwaacha maelfu ya wengine bila makaazi.