1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Kisiwa cha Migingo

13 Mei 2009

Mabishano juu ya Kisiwa cha Migingo kilioko katika Ziwa Victoria ni mali ya nani, Kenya au Uganda, bado yanaendelea.

https://p.dw.com/p/HpFI
Rais Yoweri Museveni asema Kisiwa cha Migingo ni cha Kenya na maji ni ya UgandaPicha: dpa


Tamko la karibuni la Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ni kwamba kisiwa hicho ni cha Kenya, lakini maji yanayozunguka kisiwa hicho ni ya Uganda. Kuna wabunge huko Kenya, hasa kutoka eneo la Nyanza, wanaotaka kuwahimiza wananchi wachukue hatua ya kukimiliki kisiwa hicho, ikiwa mkuu huyo wa Uganda atasita sita kuhusu jambo hilo.

Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na waziri wa nchi katika wizara ya mambo ya kigeni ya Uganda, Okello Oryem, kutaka ufafanuzi kutoka kwake kuhusu matamshi ya Rais Museveni:


Mwandishi: Othman Miraji

Mhariri: Mohamed Abdulrahman