1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa serikali ya Tcheki

Oumilkher Hamidou26 Machi 2009

Kishindo cha ndani cha jamhuri ya Tcheki cha tishia kuutikisa Umoja wa ulaya

https://p.dw.com/p/HJyx
Waziri mkuu wa jamhuri ya Tcheki Mirek TopolanekPicha: AP


Mada kuu zilizohanikiza magazetini hii leo ni pamoja na hatua za serikali kuu ya Ujerumani dhidi ya picha zinazowaonyesha watoto wakiwa uchi katika mitandao ya internet na kurefushwa muda wa watu kulipwa fidia wanapokubali kuachana na magari yao makongwe.Kuhusu siasa ya nje,kizungumkuti kinachoikumba jamhuri ya Tcheki ndicho kilichopewa umbele na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.


Tuanzie na mada hiyo ya siasa ya nje kwa maoni ya gazeti la NÜRNBERGER ZEITUNG linaloandika:


Baada ya kung'olewa madarakani waziri mkuu Mirek Topolanek,sio peke yao wacheki wanaojikuta bila ya nahodha,Umoja wa Ulaya pia utatikiswa na athari za hali hiyo.Na mtihani huu umetokea wakati mbaya kabisa;Barack Obama anapanga kuwatembelea wazungu wa ulaya mapema mwezi wa April,mkutano wa kilele wa kundi la G-20 kuhusu mgogoro jumla wa kiuchumi na fedha unakurubia na zaidi ya hayo uchaguzi wa Ulaya pia unatazamiwa kuitishwa mwezi June mwaka huu.Lakini yote hayo wabunge wa jamhuri ya Tcheki hayawashughulishi.Wamempigia kurea ya kutokua na imani kiongozi wa serikali,anaejikuta kati kati ya wadhifa wake wa zamu kama mwenyekiti wa umoja wa Ulaya.Huko sio kuwajibika hata kidogo."


Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linahofia kung'olewa madarakani TOPOLANEK kusije kukaathiri pia utaratibu wa kuufanyia marekebisho Umoja wa ulaya.Gazeti linaendelea kuandika:


Yadhihirika kana kwamba mgogoro wa fedha na kiuchumi hauutoshi Umoja wa ulaya, unajikuta hivi sasa ukizongwa na mwengine-safari hii kuhusu mwenyekiti wake wa zamu.Ni sawa kabisa mtu akisema ni haki ya wabunge wa jamhuri ya Tcheki kumpokonya imani yao waziri mkuu,lakini kwa kuipindua serikali ya mjini Prag,wamefungua njia ya kuzidi kudhoofika juhudi za karibu miaka kumi sasa za Umoja wa Ulaya,kuzifanyia marekebisho taaasisi zake.Ikiwa licha ya Ireland ambayo bado haijaidhinisha mkataba wa Umoja wa Ulaya,Jamhuri ya Tcheki itageuka kua nchi ya pili itakayo ongozwa na mtu anaeweza kuupinga mkataba huo,basi bila ya shaka juhudi za kuzifanyia marekebisho taasisi za Umoja wa ulaya zitaingia pia hatarini.


Kuhusu siasa ya ndani,gazeti la  NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG linasifu hatua kali za serikali dhidi ya picha za uchuki za watoto katika mtandao wa internet,gazeti linaendelea kuandika;


"Ni sawa kabisa kuiona serikali ikipania kupambana na visa vya kuonyeshwa picha za uchi za watoto katika mtandao wa Internet.Muda mrefu umepita hadi wanasiasa na jamii walipoitambua hatari ya aina hii ya uhalifu wa kuandaliwa.Tangu miaka michache iliyopita ndipo hatua kali zilipoanza kuchukuliwa dhidi ya makundi ya wahalifu ya mafia yanayoendeleza visa vyao vya uhalifu kupitia watoto pia.Kwa kufungwa mitandao,hatua muhimu itakua imechukuliwa hata kama haitoshi.Lakini pekee kuzuwiliwa njia za kuingia katika mitandao inayoonyesha picha za uchi za watoto ni hatua ya maana."





Mwandishi:Hamidou Oummilkheir /DPA

Mhariri: Abdul-Rahman