1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Uchumi ukabiliwe kwa kupunguza kodi

M.Fürstenau - (P.Martin)6 Januari 2009

Viongozi wa vyama ndugu vya CDU na CSU na chama shirika serikalini SPD walikutana siku ya Jumatatu kuujadili mpango wa pili wa msaada wa serikali kufufua uchumi uliozorota.

https://p.dw.com/p/GT5E
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) sitzt am Dienstag, 30. Dez. 2008 im Bundeskanzleramt in Berlin nach der Aufzeichnung ihrer Neujahrsansprache vor einem Fenster mit Blick auf den Reichstag. Die Ansprache wird am Mittwoch, 31. Dez. 2008 um 20:10 Uhr in der ARD ausgestrahlt. (AP Photo/ Michael Gottschalk,pool) Chancellor Merkel after her New Year's Eve speech was recorded in the Berlin Chancellery on Tuesday, Dec. 30, 2008. The speech will be broadcasted on Dec. 31, 2008 in German TV. (AP Photo/ Michael Gottschalk,pool)
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.Picha: AP

Matokeo ya mwisho ya mpango huo yanatazamiwa Januari 12 viongozi hao watakapokutana kwa mara ya pili.Imechukua muda lakini sasa, Kansela Merkel wa chama cha CDU yupo tayari kukabiliana na mzozo wa uchumi kwa kupunguza kodi ya mapato. Merkel ameshinikizwa kuchukua hatua hiyo na chama ndugu cha CSU kutoka Jimbo la Bavaria,kinachounda muungano na CDU katika bunge la Berlin Bundestag.Lakini chama cha SPD kinachoshiriki katika serikali ya mseto kinang'ang'ania msimamo wake wa kupinga kupunguzwa kodi ya mapato.Kinasema,badala yake waajiriwa wapatiwe nafuu kwa kupunguziwa sehemu yao ya malipo kwa bima za huduma za kijamii.

Hadi mwisho wa mwaka ujao,mpango huu wa pili kusaidia kuimarisha uchumi,utaigharimu serikali ya Ujerumani Euro bilioni 50.Ni matumaini ya vyama tawala kuwa hadi hapo,mzozo wa fedha ulioathiri dunia nzima utadhibitiwa kwa sehemu fulani.Baada ya mkutano wa hiyo jana Merkel alisema,kuna masuala fulani yanayohitaji kujadiliwa zaidi lakini malengo yao ni mamoja yaani:

"Kuhifadhi na kutoa nafasi mpya za ajira-kuitayarisha Ujerumani kwa siku zijazo.Akaongezea:

"Ndio maana hatutouvuka tu wakati huu mgumu,bali tutaibuka imara zaidi kwa kushirikiana na makundi mbali mbali ya kijamii."

Wakati huo huo,Waziri wa Mambo ya Nje Frank-Walter Steinmeier wa chama cha SPD atakaegombea ukansela katika uchaguzi ujao,anataka kuimarisha uchumi kwa njia ya kiungwana kwa kuanzisha mfuko wa fedha kwa ajili ya miradi ya ukarabati wa shule na barabara.Kwa maoni ya chama cha upinzani cha FDP,uwekezaji katika miradi ya elimu na miundo mbinu ni njia barabara.Vile vile kila mmoja apatiwe nafuu ya kifedha kwa kuzidishiwa kiwango kischotozwa kodi ya mapato.

Juma hili wabunge watakuwa na nafasi ya kuupitia kwa kina mpango wa pili wa msaada wa serikali kufufua uchumi.Hatima ya mpango huo,itaamuliwa pale viongozi wa vyama vya serikali ya mseto watakapokutana Jumatatu ijayo.