1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NÜRENBERG: Idadi ya wakosa ajira yapunguka Ujerumani

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBwC

Idadi ya watu wanaotafuta ajira nchini Ujerumani imepunguka hadi kufikia kiwango cha chini kabisa tangu miaka mitano iliyopita.Takwimu zilizotolewa na Idara ya Ajira ya Ujerumani mjini Nürenberg, huonyesha kuwa mwezi wa Mei,watu waliokosa ajira ni milioni 3.8 yaani ni asilimia 9.1 kulinganishwa na asilimia 11 katika mwezi kama huo mwaka uliopita.