1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABLUS: Machafuko mengine yazuka Ukingo wa Magharibi

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChB
Kikao cha Mahakama za Gacaca
Kikao cha Mahakama za GacacaPicha: Deutsche Welle/Mark Caldwell

Wafuasi wa chama cha Fatah cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas, wamewafyatulia risasi wafuasi wa chama cha Hamas katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Maofisa wa hospitali na walioshuhudia wamesema watu tisa wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililofanywa wakati maelfu ya wapiganaji na wanamgambo wa Hamas walipokuwa wakifanya mkutano wa hadhara mjini Nablus.

Afisa wa chama cha Fatah amesema wanamgambo wa Hamas waliandaa mkutano huo licha ya makubaliano ya kuuahirisha. Maofisa wa usalama walio watiifu kwa rais Abbas wamepelekwa mjini Nablus kurejesha utulivu.

Wakati haya yakiarifiwa, waziri mkuu wa Palestina, Ismail Haniya, leo ametangaza kwamba amekubali miito iliyotolewa na rais Mahmoud Abbas kuanza tena mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kati ya chama cha Hamas na Fatah.

Wapambe wa Abbas hata hivyo wamesema kurejea katika mazungumzo hayo kutakuwa na maana ikiwa chama cha Hamas kitakubali masharti matatu ya jamii ya kimataifa ili kumaliza usitishwaji wa misaada ya kifedha kwa Palestina.