1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAHR AL-BARED:Majeshi ya serikali yapambana na Fatah al Islam

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtj

Jeshi la Lebanon linaendelea kushambulia ngome za wapiganaji wa kiislamu wanaojificha katika kambi ya Nahr al Bared.Kulingana na serikali wapiganaji hao wanalenga kushambulia majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa mataifa yaliyoko nchini humo.

Shambulio hilo karibu na kambi ya wakimbizi ya Nahr al Bared lilianza saa mbili asubuhi za Lebanon na bado linashika kasi kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Wapiganaji wa kundi la Fatah al Islam lililipiza kisasi kwa kufyatua riasi na kurusha makombora.Wapiganaji hao aidha wanatisha kuongeza mashambulio hayo endapo wanazidi kushambuliwa kulingana na msemaji wa kundi hilo Shahine Shahine.

Kikosi cha majeshi ya kulinda usalama cha Umoja wa mataifa kilichoimarishwa kinashika doria katika eneo la mpakani na Israel kulingana na makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa na Umoja wa mataifa kati ya Israel na kundi la Lebanon la Hezbollah.