1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar asema hakuna uwezekano wa kuundwa serikali ya mseto

7 Mei 2008

Nchini Tanzania mvutano kuhusu suala la kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar bado linaendelea kuzua mvutano.

https://p.dw.com/p/DvoV

Hapo jana Naibu Waziri Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi Ali Juma Shamhuna alinukuliwa akisema kwamba hakuna uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo.Chama cha CUF kwa upande wake kimekitaka chama tawala CCM kufafanua kauli hiyo.


Ikumbukwe ya kwamba CCM ilitoa pendekezo la kutaka kufanyika kwa kura ya maoni visiwani humo juu ya kuundwa kwa serikali ya mseto kama ilivyopendekeza kamati ya vyama viwili vya CUF na CCM katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mpasuko wa kisiasa visiwani zanzibar.

Thelma Mwadzaya aliwasiliana na Ismail Jussa ambaye ni Msaidizi Maalum wa Katibu katika Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ya chama cha CUF na kwanza alitaka kujua chama hicho kimeipokea vipi kauli hiyo ya Naibu waziri kiongozi Juma Shamuhuna.