1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Abambwa akitoroka na dola 159,000

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQG3

Manaume mmoja wa Kenya hapo jana amekamatwa akiwa kwenye kitendo cha kuiba miliono 10 na nusu za Kenya sawa na dola 159,000 katika benki aliokuwa anafanya kazi katika mji w magharibi wa Kisumu.

Mtumishi huyo wa Benki ya The Guardian alikamatwa na mifuko miwili iliosheheni fedha hizo taslimu wakati akitoroka kwa kupitia mlango wa nyuma wa benki hiyo mjini Kisumu mji ulioko kama kilomita 350 kaskazini magharibi ya Nairobi.

Mtumishi huyo alikuwa ametakiwa kuzipeleka fedha hizo katika Benki Kuu ya Kenya lakini badala yake akaamuwa kuchomoka nazo.