1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Ethiopia yaambiwa iondoshe vikosi vyake Somalia

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmz

Msemaji wa bunge la serikali ya mpito ya Somalia amesema,Ethiopia ina wanajeshi 15,000 nchini Somalia na italaumiwa kwa vita vyo vyote vitakavyotokea katika nchi hiyo yenye vurugu, kwenye Pembe ya Afrika.Sharif Hassan Sheikh Adan wa serikali ya mpito ya Somalia ambayo huungwa mkono na nchi za magharibi,anajaribu kuleta masikilizano kati ya serikali hiyo dhaifu na Muungano wa Mahakama za Kiislamu unaodhibiti maeneo mengi nchini Somalia.Ethiopia inaiunga mkono serikali ya mpito iliyo na makao yake katika mji wa Baidoa,unaozidi kujongélwa na wapiganaji wa Muungano wa Kiislamu.Adan amesema, ili kuepusha vita,Ethiopia inapaswa kuondosha vikosi vyake bila ya masharti na kuunga mkono majadiliano yanayoendelea hivi sasa kati ya pande mbili za Kisomali.Addis Ababa lakini inakanusha kuwa ina vikosi vyake ndani ya mpaka wa Somalia.