1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. FIFA yaifungulia Kenya.

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKl

Shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu duniani FIFA jana Ijumaa imeondoa marufuku dhidi ya nchi ya Kenya kushiriki katika mchezo huo duniani, adhabu iliyotolewa kwa nchi hiyo zaidi ya miezi mitano iliyopita kwa kushindwa kuheshimu sheria za shirikisho hilo.

Katika taarifa , FIFA imesema kuwa uamuzi wa kuondoa marufuku hiyo inafuatia maendeleo muhimu katika taifa hilo la Afrika mashariki baada ya ziara ya ujumbe wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF mjini Nairobi hivi karibuni.

Ujumbe wa CAF ulioongozwa na makamu wake wa rais Amos Adamu ulipata hakikisho kutoka kwa serikali ya Kenya la kutoingilia katika uendeshaji wa shirikisho la kandanda nchini Kenya KFF , imesema taarifa ya FIFA.