1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Mafuriko yasababisha watalii kuokolewa.

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyx

Kiasi watalii 100 kutoka mataifa ya nje wameondolewa jana kutoka katika hoteli za kifahari kaskazini mwa Kenya wakati mvua kubwa zinaendelea kulishambulia eneo hilo, na kusababisha mafuriko yaliyoleta maafa.

Wakati mvua kubwa zikiendelea kulikumba eneo la kaskazini na bahari ya Hindi nchini Kenya tangu wiki iliyopita, maafisa wamesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko imepanda na kufikia watu 15 kutoka idadi iliyotangazwa siku ya Jumatano ya watu 10 na kwamba maelfu kadha ya watu hawana mahali pa kuishi.

Katika eneo la kaskazini kati la Isiolo, ambalo ni eneo maarufu la kitalii ambao wanataka kuona wanyama katika mbuga tatu za hifadhi ya wanyama mto Ewasi Nyiro ulifurika hadi katika hoteli mbili za kitalii.