1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Wanaharakati wapinga utandawazi waandamana mjini Nairobi, Kenya.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZ9

Maelfu ya wanaharakati wanaopinga utandawazi waliandamana kupitia mtaa mkubwa zaidi wa kimaskini, mwanzoni mwa kongamano la dunia la kijamii, mjini Nairobi, Kenya.

Wanaharakati hao walitoa wito wa kutatuliwa mizozo na pia kuanzishwa harakati mpya za kukabiliana na umasikini.

Mkutano huo unaendelea mjini Nairobi siku chache kabla ya mkutano wa dunia wa kiuchumi unaowajumuisha viongozi wa kisiasa na kibiashara kuanza mjini Davos, Uswisi.

Kikao hicho cha dunia cha kijamii kilianzishwa mwaka elfu mbili na moja kupingana na kikao cha dunia cha kiuchumi.

Mkutano huo wa Nairobi ndio wa kwanza kuandaliwa barani Afrika na umelenga kushughulikia maswala kadha yanayoathiri bara hilo kuanzia Ukimwi, msamaha wa madeni na utatuzi wa mizozo.

Washiriki kiasi elfu themanini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.