1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Washukiwa uhalifu wa 1994 wasipelekwe Rwanda

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ag

Shirika la Amnesty International limetoa mito ya kutowapeleka mahakamani Rwanda,wale wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu wakati wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini humo.Shirika hilo limesema,licha ya kuwepo maendeleo katika mfumo wa kisheria nchini Rwanda,lina wasi wasi ikiwa Kigali itaweza kuchunguza na kuendesha kwa haki na bila ya upendeleo,kesi zinazohusika na uhalifu wa mauaji.

Kwa mujibu wa Amnesty International,Rwanda imeziomba Uingereza,Kanada,Uholanzi,Ufaransa na Finland kuwarejesha nchini Rwanda watu kadhaa wanaotuhumiwa mauaji ya halaiki,uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mwaka 1994.