NAIROBI: Watalii 100 wahamishwa kufuatia mvua kubwa
27 Oktoba 2006Matangazo
Watalii takriban 100 kutoka Marekani, Ulaya na Japan walihamishwa jana kutoka kambi ya watalii ya Larsen na hoteli ya Samburu mjini Isiolo, yapata kilomita 200 kaskazini mwa Nairobi.
Watalii hao walihamishwa baada ya hoteli zao kufunikwa na maji baada ya mto wa Ewaso Nyiro ulio karibu kufurika kufuatia mvua kubwa.
Huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo ya kaskazini na mkoa wa pwani,idadi ya watu waliokufa maji imepanda kutoka watu watano na kufikia 15.
Maelfu ya wananchi wamehamishwa baada ya nyumba zao kusombwa au kufunikwa kabisa na maji.