1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Kiongozi mmoja wa Mungiki ashtakiwa

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWN

Kiongozi mmoja wa kundi lililopigwa marufuku la Mungiki linalolaumiwa kusababisha mauaji kadhaa mwaka huu ameshtakiwa kwa kuuza dawa za kulevya.Peter Njoroge Kamunya huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 14 endapo atapatikana na hatia ya kuuza misokoto 42 ya bangi .Mashtaka hayo hayajumuishi shughuli za kundi hilo la Mungiki zilizodaiwa kufanyika katika hati ya kukamatwa ya awali.

Kulingana na wakili wake Evans Ondieki kesi hiyo inapaswa kufutwa kwani Bwana Kamunya alizuiliwa na polisi kwa saa 24 bila kuwa na mawasiliano yoyote bila kushtakiwa.Hilo anaongeza linakiuka haki zake za kikatiba.

Jaji Helen Wasilwa aliwasilisha kesi hiyo kwa mahakama kuu na kumuachia kwa dhamana ya euro alfu 2200.Njenga Kamunya anadaiwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa kundi la Mungiki linalolaumiwa kusababisha mauaji ya afisa 15 wa polisi katika kipindi cha mwezi Arili hadi Juni aidha raia 27 wa kawaida katika kipindi cha mwaka mmoja.Wengi wao walichinjwa.Bwana Kamunya amekuwa akikwepa kukamatwa na polisi tangu mwezi Aprili baada ya polisi kutoa hati ya yeye na wengine wawili kukamatwa ambao kwa sasa wanazuiliwa.