1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI.Ubalozi wa Marekani watoa tahadhari kwa raia wake

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUJ

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetowa tahadhari kwa raia wake dhidi ya kufanya safari nchini humo kufuatia hali ya usalama inayozidi kuzorota.

Ubalozi huo umetoa tahadhari na kusema kwamba ujambazi umeongezeka nchini Kenya huku serikali ya nchi hiyo ikiwa haina uwezo wa kudhibiti hali hiyo.

Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia mfululizo wa visa vya kutekwa nyara magari.

Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la CARE ni miongoni mwa watu waliouwawa wakiwemo wanawake wawili wa kimarekani waliokuwa pamoja nae.

Marekani hata hivyo ilii orodhesha Kenya katika tahadhari za usafiri kwa miaka kadhaa sasa hata ingawa hapo awali sababu kubwa ilikuwa ni ugaidi.