1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Waasi wa Darfur wasusia mazungumzo

25 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cy

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anaeshuhgulikia mgogoro wa Darfur ametoa mwito kwa waasi wa jimbo hilo wahudhurie mazungumzo juu ya kuleta amani yaliyopangwa kufanyika nchini Libya mwishoni mwa wiki hii. Mjumbe huyo Jan Eliasson amesema kushindwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha mchakato wa hatari.

Taarifa ya Umoja wa Matifa imeeleza kuwa wawakilishi wa vyama muhimu vya waasi wa Darfur wanakusudia kususia mazungumzo hayo.

Eliasson amesema mazingira ya hatari yanaweza kutokea ikiwa fursa ya mazungumzo hayo itapotezwa.