1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kuchukuwa hatua thabiti dhidi ya umwagaji damu Kosovo

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYts

BRUSSELS

Mawaziri wa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO wako mjini Brussels Ubelgiji kuzungumzia hali ya Kosovo kufuatia kusambaratika kwa mazungumzo juu ya hatima ya jimbo hilo la Serbia.

Katibu Mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer amesema jumuiya hiyo ya nchi wanachama 26 itachukuwa hatua thabiti dhidi ya yoyote yule anayeamuwa kutumia nguvu.NATO inaongoza kikosi cha wanajeshi 17,000 kulinda amani huko Kosovo.

Wiki iliopita kundi la pande tatu la Umoja wa Ulaya ,Urusi na Umoja wa Mataifa limetangaza kushindwa kwa mazungumzo ya juu ya mustakbali wa jimbo hilo la Kosovo ambapo Waalbania walio wengi kwenye jimbo wanataka uhuru wakati Serbia ikitaka lipewe mamlaka makubwa ya utawala wa ndani.

Urusi imetishia kutumia kura yake ya turufu kuzuwiya hatua yoyote ile ya kupatiwa uhuru kwa jimbo hilo kupitia Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Serbia imeutaka Umoja wa Mataifa utowe muda zaidi wa kufikiwa muafaka kwa mzozo huo.