1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaitaka Ujerumani kutoa wanajeshi zaidi kwa Afghanistan

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzMK

BERLIN:

Ushirika wa umoja wa kujihami wa nchi za magharibi wa NATO,umeitaka Ujerumani kutuma majeshi nchini Afghanistan.Kikosi cha wanajeshi 250 wa Ujerumani kitachukua pahala pa kikosi cha Norway,ambacho kitaondoka Afghanistan wakati wa kipindi cha kiangazi.Msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Ujerumani mjini Berlin amesema kuwa Kansela Angela Merkel atakutana mwezi ujao na baraza lake la mawaziri ili kujadilia ombi hilo.Kwa mda huohuo waziri wa Ulinzi wa Ujerumani-Franz Josef Jung yuko nchini Afghanístan kwa mazungumzo.Akiwa mjini Kabul waziri huyo atakutana na rais Hamid Karzai pamoja na maofisa mbalimbali. Wizara ya Ulinzi haikutoa maelezo zaidi kutokana na sababu za kiusalama.Ujerumani ina wanajeshi zaidi ya elf 3 nchini Afghanistan kama sehemu ya kikosi cha kimataifa cha msaada kikiongozwa