1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi nne za SADC zakubaliana na umoja wa ulaya

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSxJ

Bruxelles:

Nchi nne za kusini mwa Afrika,zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi pamoja na Umoja wa ulaya.Lengo la mkataba huo ni kurahisisha shughuli za kiuuchumi kati ya nchi hizo na Umoja wa ulaya.Kamishna wa umoja wa ulaya anaeshughulikia masuala ya biashara Peter Mandelson ameutaka mkataba huo kua “ni hatia ya kihistoria” katika uhusiano kati ya umoja wa ulaya na nchi za kusini mwa Afrika.Mkataba huo umefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya umoja wa ulaya na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC.Katika awamu ya kwanza , mkataba huo ambao haukufafanuliwa unazihusu nchi nne tuu za kusini mwa Afrika,Botswana,Lesotho,Mosambik na Swaziland.Afrika kusini na Nambia zinatazamiwa kuamua hivi karibuni kama zitajiunga na mkataba huo au la.Wakati huo huo jumuia ya SADC na Umoja wa ulaya wamekubaliana kuendelea na mazungumzo yao kwa lengo la kufikia makubaliano jumla ya ushirikiano wa kiuchumi hadi ifikapo mwaka 2008.