1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda zibebe sehemu kubwa ya mzigo

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXQR

Wajumbe kutoka nchi 190 wanaohudhuria mkutano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa,Bali nchini Indonesia,wamehimizwa kuonyesha uongozi wa kishupavu kuhusu mkataba mpya wa hali ya hewa.Mkataba huo utachukua nafasi ya Mkataba wa Kyoto unaomalizika 2012.

Marekani,Australia,Japan na Kanada zimetuhumiwa kuwa zinazuia maendeleo kupatikana katika ulinzi wa mazingira.Nchi hizo zinasita kukubali kuweka kiwango cha kupunguza gesi zinazochafua mazingira.Wanaharakati wanaogombea ulinzi wa mazingira wanasema,nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda zinahusika na mabadiliko ya hali ya hewa na zinapaswa kubeba sehemu kubwa ya mzigo huo.