1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ndogo iliyowabeba wafanyikazi wa UN yatoweka Kongo

2 Septemba 2008

-

https://p.dw.com/p/F90e

KINSHASA

Ndege ndogo inayoaminika kuwabeba wafanyikazi wa Umoja wa mataifa imetoweka katika ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Ndege hiyo yeye uwezo wa kubeba watu 19 ilikuwa ikisafiri kutoka mjini Kinshasa kuelekea eneo la mashariki mwa jamhuri ya kidemkrasi ya Kongo.

Ndege hiyo ilitarajiwa katua katika uwanja wa ndege wa mji wa mashariki wa Bukavu lakini hadi sasa haijaonekana na wala maafisa hawajui iko wapi.

Aidha maafisa wa Umoja wa mataifa hawana taarifa juu ya watu wangapi walikuwemo ndani ya ndege hiyo lakini inasadikiwa wafanyikazi wa ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo ni miongoni mwa wasafiri.

Shirika la ndege la Air Serve halijatoa ripoti yoyote kuhusiana na ndege hiyo.