1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’DJAMENA : Waasi wapambana na wanajeshi

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpW

Waasi wa Chad na vikosi vya serikali wamepambana mapema leo hii karibu na mji wa Abeche ulioko kilomita 700 mashariki mwa mji mkuu wa N’djamena.

Duru za kijeshi zimesema mapigano hayo yamezuka baada ya alfajiri kwenye viunga vya mji wa Abeche ambao ni mji mkubwa mashariki mwa Chad wakati jeshi lilipodukiza mkururo wa waasi.

Mawasiliano yote yale ya simu na mji huo yamekatwa mapema leo asubuhi.

Waasi wa Umoja wa Vikosi vya Maendeleo na Demokrasia UFDD hapo Ijumaa walianzisha mashambulizi mapya dhidi ya Rais Idriss Deby kwa kuingia ndani ya ardhi ya Chad kueleka Abeche wakitokea Sudan.