1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’DJAMENA :Waasi warudi mpakani mwa Sudan

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCov

Makundi mawili ya waasi nchini Chad yameondoka kutoka maeneo waliyokuweko kwenye miji ya mashariki leo hii lakini wameapa kuendeleza mashambulizi yao ya kuipinduwa serikali ya Idris Derby.

Mkururo wa waasi hao ulioripotiwa kuwa ulikuwa ukielekea katika mji mkuu wa N’djamena mwishoni mwa juma leo umerudi kuelekea kwenye mpaka na Sudan.

Duru za kijeshi za Chad zimesema mkururo huo mkubwa wa waasi hapo jana iliripotiwa kuwa ulikuwa kilomita 400 kutoka N’djamena ulikuwa unatowa tishio kwa wananchi wa mji huo hivi sasa unaelekea mashariki kwa nchi hiyo.