1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

N’DJAMENA:Waasi watimuliwa na majeshi ya serikali.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz6

Jeshi nchini Chad limewatimua waasi ambao waliishambulia miji mitatu ya mashariki siku chache zilizopita kuelekea mpakani kati ya nchi hiyo na Sudan.

Jenerali Bichara Issa Chadallah aliwaambia waandishi wa habari kwamba, miji yote ambayo waasi waliingia hivi sasa tayari imesharejeshwa mikononi mwa serikali.

Hapo jana waziri wa mambo ya kigeni wa Chad aliilaumu nchi jirani ya Sudan kwa kuwaunga mkono waasi, ambao wameingia katika nchi yao kwa kupitia jimbo la magharibi la Darfur.

Jeshi la waasi linaaminika kuwa ni kidogo zaidi ya lile lililoushambulia mji mkuu mnamo mwezi April.