1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndoto ya serikali moja kwa Afrika nzima ?

4 Julai 2007

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika umemalizika accra bila maafikiano ya kutimiza ile ndoto ya Kwame Nkrumah ya kuwa na serikali moja kwa afrika nzima.

https://p.dw.com/p/CHBf

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika “African union” umemalizika jana mjini Accra,Ghana:

Kileledni mwa agenda yake ulikuwa mradi mkubwa wa kihistoria-kuwa na serikali moja ya shirikisho kuanzia Kairo hadi Cape Town.Ndoto hii asema Ludger Schdomsky katika uhariri wake, haikutimilia.Kwani mjini Accra viongozi wa Afrika waliafikiana tu shabaha hiyo ifikiwe hatua kwa hatua.

Mwishoni matokeo ni yale yale yaliotarajiwa,suluhisho la kufuta aibu kwa pande zote.Hadi mkutano ujao wa kilele hapo januari 2008 inapangwa kutunga ramani itakayoelekeza njia ya kuundwa kwa “Muungano wa dola za Afrika.”

Muda mfupi kabla usiku wa manane hapo jana ,mwenyeji wa mkutano rais John Kufour wa Ghana alisalim amri na kukubali kushindwa juhudi zake zote za kuziba mwanya kati ya wale walioungamkono na wale waliopinga kuwa na muungano huo wa dola za Afrika hivi sasa.Wachunguzi kwenye ukumbi wa mkutano walijionea viti vya Kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi na cha rais Abdoulaye Wade wa Senegal vitupu.Walikaa kandfo lilipotolewa “Tangazo la Accra”.

Fikra ya kuwa na muungano wa dola za Afrika mfano wa Marekani, kwa kweli ni mapema.Afrika ilioungana bila shaka ingelikua mshirika anefaa katika meza ya mazungumzo na kulipa bara hilo uzito ukitia maanani utajiri wake wa mali asili na bidhaa zake za kilimo.

Pia muungano wa dola za Afrika unelipa bara hilo uzito wa kisiasa katika jukwaa la kimataifa na badala ya kuzungumza kwa sauti 53 likazungumza kwa sauti moja.

Kituo cha kuasisiwa muungano wa dola za Afrika kilifaa barabara ,kwani ni Accra,mji mkuu wa Ghana ambako marehemu Dr.Kwame Nkurumah alikoitisha Afrika ingefaa kuwa na serikali moja –rai alioitoa miaka 50 iliopita.Zama zile fikra hiyo haikufanikiwa kwavile kila taifa changa la Afrika likijivutia masilahi yake binafsi.

Na leo ishara za maafikiano ni bora isipokuwa

Hazitoshi.Ingawa muungano huo ungeweza kuegemea Umoja wa afrika uliopo sasa pamoja na Bunge lake lililoanzishwa 2004,lakini pangehitajika Bunge hilo kuwa na mamlaka ya kupitisha sheria.Pia pangehitajika katiba moja na Banki moja kuu.

Isitoshe, kuna ukosefu wa mawazo sawa miongoni mwa nchi zanachama pamoja na kutoaminiana.Kwa mfano, vipi Ethiopia na Eritrea au Sudan na Chad ziweze kutunga sera moja ya Afrika wakati kama majirani zinapigana vita ?

Uchunguzi ulioamrishwa kufanywa 2006 na Umoja wa Afrika umegundua kuwa serikali moja kwa bara zima la Afrika na soko moja la kiuchumi lingeliimarisha mno bara hilo pamoja na kutoa nafasi nyingi zaidi za kazi na kunghepunguza ufukara barani humo.

Hata wakati ulikwishaamuliwa: Hadi 2015 ni ilikua kuunda muungano wa dola za Afrika.Iliosalia ni swali:nani atakaegharimia mradi huo ? Umoja wa Afrika wenyewe takriban umefilisika,kwani ni wanachama wachache tu walipao michango yao.Je, Marekani na dola za Ulaya zichangie ?Umoja wa Ulaya tayari una mizozo yake seuze Umoja wa Afrika wenye dola 53 na wakaazi milioni 800 wenye lugha hadi 2000 mbali mbali.

Kwahivyo, ingelifaa mjini Accra kutotaka makuu ,bali kungeshughulikiwa ufumbuzi unaowezekana wa matatizo yaliopo sasa.