1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu amuonya Merkel juu ya Iran na wakimbizi

Saumu Mwasimba
5 Juni 2018

Waziri mkuu wa Israel amemuonya kansela Merkel kwamba uingiliaji kati wa Iran katika mgogoro Mashariki ya kati unaweza kusababisha wimbi la wakimbizi kuelekea Ulaya

https://p.dw.com/p/2yx7v
Berlin Deutsch-Israelische Regierungskonsultationen Netanjahu Merkel
Picha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Gazeti la «Rhein-Neckar-Zeitung» kutoka (Heidelberg) linazungumzia mkutano wa Merkel na Netanyahu pamoja na mtizamo wa Umoja huo katika suala la mgogoro wa Mashariki ya Kati. Mhariri anaandika kwamba.

Kansela Angela Merkel siku ya Jumatatu kwa kiasi fulani ameonesha kufanikiwa kuubadilisha mtizamo wa Ujerumani katika kuuzungumzia mgogoro wa Mashariki ya Kati na sio tu katika kumtetea Netanyahu lakini pia kama msuluhishi katika mgogoro huo. Pamoja na hilo lakini hamasa itaonekana pale tu Umoja wa Ulaya utakapoanza kuichanganua upya dhima yake kama mtukati au msuluhishi katika mgogoro huo. Hapo ndipo Mashariki ya kati itakapoweza kuona mafanikio.

Mhariri wa gazeti la «Leipziger Volkszeitung» kuhusu ziara ya Netanyahu Ujerumani anaandika.

Mwelekeo sahihi wa sera sio tu unaoangalia kuvunjika moyo kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Hapana shaka kwamba Israel ilikuwa na matarajio makubwa zaidi kutoka kwa rafiki ambaye hususan ameendelea kuonesha uwajibikaji kwa nchi hiyo. Ujerumani sio nchi yenye nguvu kubwa za kijeshi lakini inaweza kuwa na nguvu kutokana na dhima yake barani Ulaya na nguvu zake kiuchumi inaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kubeba jukumu la kuwa msuluhishi. Hakuna lakini lugha ya uwazi inayoweza kueleweka Jerusalem na Teheran.

Gazeti la «Leipziger Volkszeitung» limejikita kuzungumzia mageuzi barani Ulaya,mhariri anasema.

Ulaya inahitaji kuchukua hatua zaidi ikiwa inataka kujiondoa katika mgogoro unaoukabili. Unahitaji ujasiri zaidi na mwelekeo barabara. Na pia hapana shaka fedha zaidi kutoka Ujerumani. Suala hapa sio kuhusu mfumo mbaya wa sera katika nchi za Ulaya ya kusini ambazo zinapata mabilioni ya ruzuku zinazotokana na fedha za walipa kodi wa kijerumani. Suala hapa zaidi linahusu uwekezaji katika mustakabali wa Ulaya. Na kwa mujibu wa mtazamo wa Ujerumani inawezekana fedha kutumika vizuri na faida ikapatikana.

Eppan DFB WM Trainingslager Südtirol Jogi Löw
Picha: Getty Images/Bongarts/A. Hassenstein

Mhariri wa «Badische Neueste Nachrichten» anazungumzia kikosi cha timu ya taifa ya soka  Ujerumani itakayocheza kombe la dunia nchini Urusi.Anasema

Kikosi cha Joachim Loew cha kulitetea taji la kombe la dunia la kandanda nchini Urusi kimepangika na kiko imara. Ikiwa ni imara vya kutosha kuweza kulitwaa kombe hilo dhidi ya Wafaransa wanaokwenda kasi, Wahispania waliyojiimarisha zaidi  na Wabrazili au hata timu nyinginezo zinazoonekana kuwa na mafanikio zinazoweza kuwa katika nafasi nzuri katika michuano hiyo inayooanza Juni 17. hilo litakapodhihirika katika mchezo wa kwanza wa timu hiyo ya Ujerumani katika kundi lake ambapo itacheza na Mexico.

Mhariri wa gazeti la «Badische Zeitung» kuhusu timu ya Ujerumani itakyokwenda Urusi.

Joachim Low ameshaamua kikosi chake,Nils Petersen hatokwenda nchini Urusi kuwa pamoja na kikosi hicho cha timu ya taifa ya Ujetrumani na hilo halikushangaza. Ilishadhihirika tangu mwanzo kwamba yeyote ambaye hakuwahi kuwa na nafasi yoyote ya kucheza hadi hivi karibuni katika timu hiyo ya taifa ya Ujerumani hatoorodheshwa. Kwahivyo hata uamuzi wa mkufunzi huyo wa timu ya taifa kuelekea  Peterson haupaswi kutafsiriwa vingine. Kwa Low kuwazungumzia vibaya baadhi ya wachezaji wake ni kitu kilichokuja katika wakati mwafaka.

Mwandishi: Saumu Yusuf

Mhariri: Grace Patricia Kabogo