1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI.Mvua kubwa yasababisha uharibu mkubwa Bangladesh

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs2

Mvua kubwa inayoambatana na upepo mkali iliyosababisha uharibifu nchini Bangladesh imeingia katika nchi jirani ya India na kusababisha vifo na kutatiza shughuli za usafiri.

Maafisa wanasema watu kadhaa wameuwawa kwenye ajali zilizosababishwa na mvua hiyo mashariki mwa nchi.

Wakati huo idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya matope katika mji wa bandari wa Chittagong huko Bangladesh imepanda na kufikia watu 119.

Watu zaidi ya millioni tano nchini humo wanakabiliwa na kitisho cha kuathiriwa na mafuriko yanayosabishwa na mvua.