1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban Ki Moon azitaka Marekani na Uingereza ziwe na subira

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwW

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amezitolea mwito Marekani na Uingereza ziwe na subira kabla kuwasilisha pendekezo la kuiongezea vikwazo Sudan kwa baraza la usalama la usalama la Umoja wa Mataifa.

Ban Ki Moon aliwaambia waandishi wa habari katika makao ya makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, kwamba anahitaji muda zaidi kuishawishi serikali ya Sudan ikubali kikosi cha kulinda amani kitakachojumulisha wanajeshi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenda Darfur.

´Kuhusu vikwazo na diplomasia nadhani kunaweza kuwa na ushirikiano. Ipo haja, ikizingatiwa jinsi serikali ya Sudan ilivyokuwa ikiushughulikia mzozo wa Darfur, kuendelea kuibinya.´

Hapo awali katibu mkuu Ban Ki Moon alimkosoa vikali rais wa Marekani, George W Bush, kwa uamuzi wake wa kuiwekea vikwazo vipya serikali ya Sudan.

Hapo jana rais Bush alitangaza ataongeza vikwazo dhidi ya Sudan kuibinya ikomeshe umwagaji damu unaoendelea katika jimbo la Darfur.

China, Misri na jumuiya ya nchi za kiarabu pia zimeikosoa Marekani kwa kuiwekea vikwazo Sudan.