1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la usalama kumpigia kura mrithi wa Annan

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4d

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linajiandaa kumchagua mrithi wa katibu mkuu wa umoja huo, Kofi Annan, wakati wa kikao maalum hii leo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya Kusini, Ban Ki-Moon anapigiwa upatu kuungwa mkono na baraza hilo.

Kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa, wanachama 15 wa baraza la usalama watawasilisha pendekezo lao kwa baraza kuu lenye wanachama 152, ambalo lazima liidhinishe kabla katibu mkuu kuchukua madaraka.

Ban Ki-Moon ni mgombea pekee aliyesalia katika kinyang´anyiro cha kuwania wadhifa wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.