1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York :Baraza la usalama launga mkono kikosi cha kimataifa Darfur

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChm

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa,limeunga mkono kuundwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika- AU, kwa ajili ya kusimamia amani katika jimbo la magharibi mwa Sudan-Darfur. Wakati Sudan inapinga kutumwa kwa kikosi cha kimataifa jimboni humo, Katibu mkuu wa umoja huo Kofi Annan akizungumza mjini New York ameelezea matumaini ya kupatikana maelewano.

Wakati huo huo baraza la usalama limezitaka pande zote zinazohusika kukiimarisha kikosi cha umoja wa Afrika kilicho hivi sasa Darfur. Taarifa ya baraza hilo ilisema juhudi za kukiimarisha kikosi cha umoja wa Afrika cha wanajeshi 7,000 hazina budi zianze mara moja.