1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Feruji yakwamisha shughuli katika sehemu ya New York- Marekani

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2N

Zaidi ya watu 320,000 hawana umeme na shughuli zimekwama katika jimbo la New York nchini Marekani kufuatia feruji nyingi ilioanguka katika eneo la kando kando ya kiunga cha Buffalo.

Feruji hiyo ambayo imefikia sentimeta 60 kutoka ardhi, ilikuwa nyingi kuwahi kutokea kwa muda wa miaka 140 iliopita na wataalamu wa hali ya hewa wanahofia kutokea mafuriko makubwa wakati feruji hiyo itakapotoweka.