1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Gambari kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Irak

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMk

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon amemteua mwanadiplomasia wa Kinigeria kama mjumbe wake maalum,kuhusika na misaada ya umoja huo kuijenga upya Irak.Ibrahim Gambari,ataratibu misaada ya Umoja wa Mataifa kwa Irak kuambatana na mradi wa ushirikiano uliokubaliwa mwezi wa Julai mwaka 2006.Umoja wa Mataifa,katika kipindi cha miaka mitano ijayo,kwa idhini ya Benki Kuu ya Dunia,unatazamia kusaidia kazi za kuijenga upya Irak.