1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Haysom kuongoza masuala ya kisiasa

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1N

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua wakili kutoka Afrika ya Kusini kuwa mkurugenzi wa masuala ya kisiasa katika ofisi yake.Nicholas Haysom aliwahi kumhudumia rais wa zamani wa Afrika ya Kusini,Nelson Mandela,baada ya kuchaguliwa kama mshauri wake wa kisheria mwaka 1994.Haysom alishiriki katika majadiliano yaliyohusika na katiba ya Afrika ya Kusini baada ya kuondoshwa utawala wa ubaguzi wa kikabila.