1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Iraq yashutumiwa kwa kuficha maafa ya raia

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC78

Umoja wa Mataifa umeishutumu serikali ya Iraq kwa kufanya siri idadi halisi ya maafa ya raia nchini humo.

Katika repoti yake ya hivi karibuni ya haki za binaadamu ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Iraq umeitaka serikali ya Iraq kujiendesha kwa njia ya uwazi zaidi.Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ameushutumu Umoja wa Mataifa kwa kuongezea chumvi idadi ya vifo vya raia na kusema kwamba jambo hilo linatowa picha mbaya kwa rekodi yake ya haki za binaadamu.

Umoja wa Mataifa unasema watu 34,000 wameuwawa kutokana na mashambulizi hapo mwaka 2006 na kwamba wananchi wengine wa Iraq 70,000 wamezikimbia nyumba zao kukwepa umwagaji damu.

Maliki anapinga takwimu hiyo.