1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Sudan kuchunguza bughdha iliyotendwa dhidi ya wafanyikazi wa Umoja huo.

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCY5
Uchumi unaendelea kuboreka nchini Ujerumani
Uchumi unaendelea kuboreka nchini UjerumaniPicha: AP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuchunguza kitendo cha juma lililopita cha kukamatwa na kujeruhiwa wafanyakazi 20 wa Umoja huo wanaotoa misaada katika eneo la Darfur.

Ban Ki-Moon amesema maafisa wa usalama wa Sudan waliwavamia na kuwakamata wafanyikazi hao katika mji wa Nyali, kusini mwa Darfur.

Makao ya Umoja huo nchini Sudan yamearifu baadhi ya wafanyi kazi hao walijeruhiwa wakati waliposhikiliwa kwa muda.

Umoja wa Mataifa umesema utawasilisha rasmi malalamishi kwa serikali ya Sudan kwa kukiuka sheria za kimsingi.