1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, akataa wito wa Marekani aongeze idadi ya watumishi wa Umoja huo nchini Iraq.

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZr

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekataa wito wa Rais George Bush wa Marekani kuongeza idadi ya watumishi wa Umoja huo nchini Iraq.

Ban Ki-Moon amesema shughuli za Umoja huo zimetatizwa kwa kiasi kikubwa nchini Iraq kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo, Ban Ki-Moon aliahidi kwamba Umoja huo utaendelea na mkakati wake wa kusaidia ukarabati wa Iraq kwa nia ya kuleta mageuzi ya kidemokrasia nchini humo.

Katibu Mkuu huyo alikuwa akihutubia waandishi wa habari alipowasili kutoka Washington alikoshauriana na Rais George Bush pamoja na wabunge.