1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mabaki ya maiti yapatikana mjini NewYork

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0b

Mabaki ya maiti za watu yamepatikana mjini New York katika eneo la mashambulio ya Septemba 11 mwaka wa 2001 dhidi ya Marekani. Wafanyakaziw a ujenzi wamegundua mifupa inayoaminiwa kuwa ya waathiriwa wa mashambulio dhidi ya jengo la shirika la kibiashara la kimataifa, WTO.

Kufuatia kupatikana kwa mabaki hayo, maofisa wa mji wa New York wameamua kufanya uchunguzi zaidi katika eneo hilo kutafuta mabaki mengine.

Watu takriban elfu 27 waliuwawa katika mashambulio hayo dhidi ya jengo hilo mjini New York na zaidi ya 1,000 hawajapatikana mpaka leo.