1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Marekani kulaani kukanusha mauaji ya halaiki ya wayahudi

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYX

Marekani imeandaa pendekezo la azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kulaani kukanusha mauaji ya kiholela dhidi ya wayahudi.

Azimio hilo halitaji taifa lolote lakini limetayarishwa mwezi mmoja tangu Iran ilipoandaa mkutano ambapo washirika wa mkutano huo walihoji ikiwa mauaji ya halaiki ya wayahudi yalifanyika au yalitiliwa chumvi.

Msemaji wa tume ya Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema azimizo hilo linawasilishwa kuenda sambamba na maadhimisho ya kimataifa ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya halaiki yatakayofanyika tarehe 27 mwezi huu.