1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mataifa makubwa dunia yauangalia kwa kina mzozo wa Darfur

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLD

Mataifa makubwa yenye nguvu duniani, yameanza kuangalia njia za kuchukua ili kumshawishi Rais wa Sudan, akubali jeshi la pamoja la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kusaidia kurejesha amani katika eneo la Darfur.

Nchi hizo ambazo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pia zinaangalia hatua gani zitachukua iwapo ushawishi wao utashindwa.

Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Emry Jones Parry, amesema kuwa nchi hizo zinaangalia kwa kina jinsi ya kumshawishi Rais Omar Hassan Al Bashir akubali kuwepo kwa jeshi hilo.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameongeza kasi katika juhudi za umoja huo kupeleka kikosi cha askari elfu 24 cha kulinda amani huko Darfur.

Katika juhudi mpya za kuutanzua mzozo huo wa Darfur, Ban Ki-Moon amemuandikia barua, Rais Al Bashir wa Sudan, kumuelezea juhudi hizo mpya.