1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mwanariadha akiri kuchukua dawa kuongeza nguvu

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IA

Mwanariadha Marion Jones wa Marekani amekiri kuchukua dawa za kuongeza nguvu.Baada ya kukiri mahakamani mjini New York,mwanariadha huyo aliomba msamaha kwa umma.Katika michezo ya Olimpik ya mwaka 2000 mjini Sydney,Jones alishinda medali tatu za dhahabu na mbili za bronzi.