1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Uamuzi upitishwe kuhusu hatima ya Kosovo

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsV

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon ametoa wito kwa Baraza la Usalama lipitishe kwa haraka azimio kuhusu hatima ya kisiasa ya jimbo la Kosovo la Serbia.Kwa maoni ya Ban,Baraza la Usalama litaweza kupitisha uamuzi wa haki na ulio barabara,kuambatana na ripoti ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Martti Ahtisaari.Mzaliwa wa Finnland.Ahtisaari,amependekeza jimbo la Kosovo, chini ya usimamizi fulani,lipewe uhuru.